BOTI ILIYOBEBA WAKIMBIZI YAZAMA USIKU WA KUAMKIA

TAREHE 09-10-2017

Boti iliyokuwa imewabeba wakimbizi wa jamii ya Rohingya wanaokimbia machafuko katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar imezama usiku wa kuamkia leo karibu na pwani ya Bangladesh na kusababisha watu wawili kufa maji na wengine kadhaa hawajulikani walipo.

Walinzi na maafisa wa pwani wamesema boti hiyo ilikuwa imefurika watu karibu 100 wakati ilipozama katika mto Naf unaoitenganisha Myanmar na taifa jirani la Kusini mwa Asia, Bangladesh.
Operesheni ya uokozi imeendelea asubuhi hii na idadi ya watu ambao wamekosekana haijatambulika.


 Zaidi ya wakimbizi laki tano  wa jamii ya wachache ya waislamu wa Rohingya wameikimbia Myanmar tangu Agosti 25 wakati wanamgambo wa Rohingya walipowashambulia polisi na jeshi katika jimbo la Rakhine na baadaye kudhibitiwa katika operesheni kali na vikosi vya usalama vya Myanmar.
BOTI ILIYOBEBA WAKIMBIZI YAZAMA USIKU WA KUAMKIA BOTI  ILIYOBEBA  WAKIMBIZI  YAZAMA USIKU WA KUAMKIA Reviewed by safina radio on October 09, 2017 Rating: 5

No comments