MKURUGENZI MANISPAA YA TABORA ATAKIWA KUREJESHA VIWANJA

TAREHE 11-10-2017

Naibu Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mh Angelina Mabula amemwagiza Mkurugenzi  wa Manispaa ya Tabora Bw John Bosco kurejesha viwanja mbalimbali kwa wamiliki ambavyo vimemilikishwa kwa watu binafsi.

Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo kufuatoa wataalamu wa ardhi kukiuka madili ya kazi na kugawa kiwanja kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja na hivyo kutakiwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na ukiukaji huo wa maadili ya kazi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanry ametoa wito kwa watumishi waliogawa kiwanja zaidi ya mtu mmoja kuchukuliwa hatua za kisheria.
MKURUGENZI MANISPAA YA TABORA ATAKIWA KUREJESHA VIWANJA MKURUGENZI MANISPAA YA TABORA ATAKIWA KUREJESHA VIWANJA Reviewed by safina radio on October 11, 2017 Rating: 5

No comments