WATU WANNE WAMEUAWA KATIKA VURUGU ZA UCHAGUZI NCHINI KENYA
TAREHE 27-10-2017
Takriban watu wanne wameuwawa katika vurugu
za uchaguzi nchini Kenya huku Kura zikiendelea kuhesabiwa katika kituo kikuu
cha kujumlisha kura katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi baada ya marudio ya uchaguzi wa urais yalifanyika hapo
jana.
Hali ya kutokuwepo na usalama
imesababisha kuahirishwa kwa uchaguzi katika kaunti nne huku maafisa wa
uchaguzi wakisema kuwa zoezi hilo lilifanyika kwa amani na kama lilivyopangwa.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya inakadiria kuwa
asilimia 40 ya wapiga kura walijitokeza kushiriki katika zoezi hilo
ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura walioshiriki katika uchaguzi
uliofanyika Agosti 8 na ambao ulibatilishwa na mahaka ya juu ya nchini humo.
Wafuasi wa upinzani hawakushiriki
kwenye uchaguzi wa jana baada ya kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga
kuwatolea mwito wafuasi wa upinzani wasishiriki kwenye zoezi la kupiga kura.
WATU WANNE WAMEUAWA KATIKA VURUGU ZA UCHAGUZI NCHINI KENYA
Reviewed by safina radio
on
October 27, 2017
Rating:

No comments