JIMBO LA KATALONIA NCHINI UHISPANIA LAENDELEZA HARAKATI ZA KUTAKA KUJITENGA
TAREHE 02-10-2017
Jimbo la Kaskazini Mashariki mwa
Uhispania, Catalonia,lenye idadi ya watu milioni 7.5 na lenye utajirri mkubwa
unaolingana na wa nchi ya Ureno limepiga kura ya maoni kujitenga na Serikali
Kuu ya Uhispania
Kiongozi wa Jimbo hilo Bw.Carles
Puigdemont amasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia
kura ya maoni yenye utata ambayo imekumbwa na ghasia.
Maafisa wa Jimbo hilo la Catalonia
wamesema kuwa asilimia 90 ya wale walioapiga kura wameunga mkono uhuru wa Jimbo
lao katika kura ya maoni ya hapo jana jumapili.
Hata
hivyo Mahakama ya katiba nchini Uhispania imeitangaza kura hiyo ya maoni kuwa
kinyume na sheria,ambapo pia mamia ya watu wamejeruhiwa wakati polisi walitumia
nguvu kujaribu kuzuia zoezi hilo.
JIMBO LA KATALONIA NCHINI UHISPANIA LAENDELEZA HARAKATI ZA KUTAKA KUJITENGA
Reviewed by safina radio
on
October 02, 2017
Rating:

No comments