MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA GOBA MADALE DAR ES SALAAM ATAKIWA KUZINGATIA VIWANGO
TAREHE 04-10-2017
![]() |
WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MH. MAKAME MBARAWA MNYAA |
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mh Makame
Mbarawa amewataka wakandarasi wanaojenga barabara ya Goba Madale jijini
Dar-es-salaam kuzingatia viwango na ubora katika ujenzi wa barabara hiyo ili
idumu kwa muda mrefu.
Mh Mbarawa ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi
maaulumu wa ujenzi barabara zilizoko pembezoni mwa jiji la Dar-es-salaam,ambapo
amesema kuwa kampuni inayojenga barabara hiyo ni ya Kitanzania inayoitwa MICO
na inapaswa kujenga katika kiwango
kinachokubalika na si kufanya ubabaishaji.
Amesema kuwa,serikali pamoja na wananchi wanataka
waone barabara hiyo inakamilika kwa viwango na kama itakamilika kama
walivyokubaliana kampuni hiyo itaendelea kupewa kazi nyingi zaidi na serikali
lengo likiwa ni kuziwezesha kampuni za ndani.
Kwa upande wake mratibu wa mradi kutoka kampuni hiyo
ya Mico Bw Crispin Mwombeki amesema kuwa changamoto kubwa inayokabili kampuni
hiyo ulipaji wa fidia walioko kandokando ya barabara.
MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA YA GOBA MADALE DAR ES SALAAM ATAKIWA KUZINGATIA VIWANGO
Reviewed by safina radio
on
October 04, 2017
Rating:

No comments