IGP SIMON SIRRO AMESEMA BIASHARA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA IMEPUNGUA HAPA NCHINI

TAREHE  09-10-2017


Mkuu wa jeshi la polisi hapa nchini IGP Saimon Sirro amesema kuwa biashara na utumiaji wa madawa ya kulevya imepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na vyombo vya dola kudhibiti biashara hiyo.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya katika ziara yake ya kutembelea mikoa ya nyanda za juu kusini yenye lengo la kuangalia hali ya usalama katika mikoa hiyo.

Amesema kuwa tangu kuanza kwa operesheni ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini watumiaji wake wamepungua kwa kiasia kikubwa,na jeshi la polisi litaendelea kuwakamata wale wote wanaojihusisha na dawa hizo bila kujali uwezo wake wa kifedha wala cheo chake.

Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo wa polisi ameviagiza vikosi vya jeshi hilo vilivyoko maeneo ya mipakani kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi.


Amesema kuwa wafanyabishara wanapokwepa kulipa kodi wanasababisha serikali kupata mapato yake hivyo kuanzia sasa jeshi la polisi limejipanga kuwafikisha katika vyombo vya dola wafanyabiashara wote wanaokwepa kodi.
IGP SIMON SIRRO AMESEMA BIASHARA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA IMEPUNGUA HAPA NCHINI IGP  SIMON  SIRRO AMESEMA  BIASHARA  NA  UTUMIAJI  WA  MADAWA  YA  KULEVYA  IMEPUNGUA  HAPA NCHINI Reviewed by safina radio on October 09, 2017 Rating: 5

No comments