SEKTA BINAFSI HAPA NCHINI ZATAKIWA KUWASILIANA MOJA KWA MOJA NA SERIKALI

TAREHE 25-10-2017
WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DK. PHILIP MPANGO
Sekta binafsi hapa nchini imetakiwa kuwasiliana moja kwa moja na serikali ili kutatua changamoto zinazowakabili badala ya kupitia wakala wa nje kwanza kwa kuwa mlango wa serikali uko wazi kwa ajili ya majadiliano na kutatua matatizo ya sekta hiyo.

Rai hiyo imetolewa na jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katika Mkutano na sekta binafsi nchini TPSF,ambapo amesema kuwa ni vema sekta binafsi ikashirikiana na sekta ya umma kwa kuwa zote zinategemeana na hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na sekta binafsi ambayo ni imara.


Hata hivyo, amesema lengo la pande zote mbili kukutana ni kuharakisha utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano kuongeza fursa za ajira, kipato cha wananchi, kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kuwa Tanzania inaongozwa na uchumi wa viwanda.
SEKTA BINAFSI HAPA NCHINI ZATAKIWA KUWASILIANA MOJA KWA MOJA NA SERIKALI SEKTA  BINAFSI  HAPA  NCHINI  ZATAKIWA  KUWASILIANA  MOJA KWA  MOJA  NA SERIKALI Reviewed by safina radio on October 25, 2017 Rating: 5

No comments