ODINGA AMETOA WITO KWA WAFUASI WAKE KUENDELEA NA MAANDAMANO
TAREHE 16-10-2017
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini
Kenya, Raila Odinga, ambaye alijitoa kwenye uchaguzi mpya wa urais wa hapo
Oktoba 26, mwaka huu amewatolea wito wafuasi wake kuendelea na maandamano licha
ya serikali kupiga marufuku maandamano hayo.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta
imepiga marufuku maandamano kwenye vitovu vya miji mikubwa, ikisema inazuia
machafuko na uharibifu wa mali.
Akizungumza na maelfu ya wafuasi wake
katika mji wa pwani wa Mombasa, Odinga ambaye juzi alikuwa London, Uingereza,
amesema alikwenda huko kuzungumzia hasa kile kinachotokea sasa nchini Kenya.
Odinga na muungano wa upinzani wa NASA
wanashinikiza kufanyika kwa marekebisho makubwa kwenye tume ya uchaguzi, IEBC,
kabla ya kuitishwa uchaguzi mwengine.
Hata hivyo hadi sasa, watu wawili
wanaripotiwa kupoteza maisha kwenye maandamano dhidi ya IEBC.
ODINGA AMETOA WITO KWA WAFUASI WAKE KUENDELEA NA MAANDAMANO
Reviewed by safina radio
on
October 16, 2017
Rating:

No comments