MAREKANI YAPELEKA MSAADA SOMALIA
TAREHE 18-10-2017
Ndege ya kijeshi ya
Marekani imetua hii leo katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu ikiwa na misaada
ya kiutu kufuatia shambulizi lililowaua zaidi ya watu 300 nchini humo.
Shambulizi hilo baya
zaidi katika historia ya Somalia na moja ya mashambulizi mabaya ulimwenguni
limewajeruhi kiasi cha watu mia nne ambapo Maafisa nchini humo wanasema watu
kadhaa bado hawajulikani walipo na idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
Wakati mazishi ya
waliouawa yakiendelea watu kadhaa waliojeruhiwa vibaya wamepelekwa Uturuki kwa
uangalizi zaidi kimatibabu, ambapo serikali ya Kenya imeahidi kuwasafirisha
majeruhi 31 kutoka Somalia hadi Nairobi kwa ajili ya matibabau zaidi.
Hali kadhalika, Kenya imepeleka tani 11 za
madawa na mahitaji mengine nchini Somalia,na Serikali ya Somalia inalishutumu
kundi la al- Shabab kwa kuhusika na shambulizi hilo ingawa kundi hilo hadi sasa
halijatoa tamko lolote.
MAREKANI YAPELEKA MSAADA SOMALIA
Reviewed by safina radio
on
October 18, 2017
Rating:

No comments