WAZIRI LUKUVI AMEWAAGIZA MAAFISA MIPANGO MIJI HAPA NCHINI KUTENGA MAENEO MAPYA YA UWEKEZAJI NA MAKAZI.

TAREHE 27-10-2017

Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi amewaagiza Maafisa wa Mipango Miji hapa nchini kutenga maeneo mapya ya makazi na maeneo ya uwekezaji katika Halmashauri zao ili kufanikisha azma ya serkali kuelekea uchumi  wa Viwanda.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo jijini Dar es salaam kwenye Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji na kuwataka wataalamu hao kutatua changamoto katika ufuatiliaji wa maendeleo ya mipango miji.

Aidha, Waziri Lukuvi ameongeza kwa Mkutano huo uwe kama Jukwaa la kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu mpya za kuandaa mipango miji itakayofanikisha uwekezaji wa maendeleo endelevu za viwanda kwa kuwa serikali ya awamu ya tano imeamua kuweka msisitizo kwenye uwekezaji wa viwanda.

Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prf. Wilbert Kombe amesema changamoto inayowakabili ni ukosefu wa rasilimali watu katika maeneo mengi ya miji.


Hata hivyo Mkutano wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji umewahusisha Wajumbe wa bodi hiyo pamoja na Wataalamu Mipango wa Miji kutoka Halmashauri mbalimbali hapa nchini.
WAZIRI LUKUVI AMEWAAGIZA MAAFISA MIPANGO MIJI HAPA NCHINI KUTENGA MAENEO MAPYA YA UWEKEZAJI NA MAKAZI. WAZIRI  LUKUVI  AMEWAAGIZA MAAFISA  MIPANGO MIJI  HAPA NCHINI KUTENGA  MAENEO  MAPYA  YA  UWEKEZAJI  NA  MAKAZI. Reviewed by safina radio on October 27, 2017 Rating: 5

No comments