MKUU WA MKOA WA TANGA BW. MARTIN SHIGELLA AIOMBA TANESCO MKOANI HUMO KUONGEZA MIUNDOMBINU.
TAREHE 06-10-2017
Mkuu wa mkoa wa Tanga Bw
Martin Shigela ameliomba shirika la umeme Tanzania TANESCO kuongeza miundombinu
ya kutosha kwa ajili kusambaza umeme wa kutosha ili kukidhi mahitaji kwa
siku za hivi karibuni kutokana na
uwekezaji mkubwa uliopo Mkoani humo.
Shigela ametoa ombi
hilo wakati akifungua mkutano wa 47 wa
Baraza Kuu la wafanyakazi wa TANESCO
uliofanyika huko Tanga ambapo amesema Serikali inaendelea na mchakato wa
kuimarisha miundombinu ya usafirishaji wa umeme
Aidha, Shingela
ameongeza kuwa miongoni mwa miradi mikubwa
ya uwekezaji unaohitaji umeme wa
kutosha ni ujenzi wa bomba la mafuta unaoendelea kutokana na kazi kubwa ya
uunganishaji na uvalishwaji wa mabomba
hayo.
Vile vile, Shingela
ameongeza kuwa umeme unahitajika kutokana na uwepo wa ujenzi wa viwanda ambapo kiwanda kimoja kinakadiriwa
kuzalisha takribani tani milioni saba kwa mwaka na kuwapo kwa mahitaji ya
uzalishaji wa simenti na nondo kwa wingi kutoka kwenye viwanda vingine kwa
ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo huku
kukiwa na uzalishaji wa nguzo za zege zinazohitaji nondo na simenti.
Hata hivyo, Mkutano wa
Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO utafanyika kwa
siku mbili.
MKUU WA MKOA WA TANGA BW. MARTIN SHIGELLA AIOMBA TANESCO MKOANI HUMO KUONGEZA MIUNDOMBINU.
Reviewed by safina radio
on
October 06, 2017
Rating:

No comments