RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AMEMWAMBIA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TAIFA HILO KUWA ANAPOTEZA MUDA WAKE KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA YA KASKAZINI

TAREHE 02-10-2017

RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP

Rais wa Marekani Donald Trump amemuambia waziri wake wa mashauri ya nchi za nje Bw. Rex Tillerson kuwa anapoteza muda wake akijaribu kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Bw.Tillerson alifichua hayo siku ya Jumamosi akisema kuwa Korea Kaskazini haitilii  maanani mazungumzo hayo.

Marekani inataka Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya silaha baada ya kufanya majaribio kadha ya makombora ya Nyuklia na kudai kufanya jaribo la bomu la haidrojeni ambalo linaweza kutundikwa kwa kombora la masafa marefu.

Mh. Trump, alisema kuwa jeshi la Marekani lilikuwa tayari kukabiliana na Korea Kaskazini mapema Mwezi Agost, saa chache baada ya waziri wake wa ulinzi kujaribu kutuliza misukosuko akisema kuwa jitihada za mazungumzo zilikuwa zinafanikiwa.


Matamshi ya rais Trump yanakuja siku moja baada ya Bw. Tillerson kufichua kuwa maafisa wa Marekani walikuwa na mawasiliano na Korea Kaskazini licha ya kuwepo vita vya maneno kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.
RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AMEMWAMBIA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TAIFA HILO KUWA ANAPOTEZA MUDA WAKE KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA YA KASKAZINI RAIS  WA  MAREKANI  DONALD TRUMP  AMEMWAMBIA  WAZIRI WA  MAMBO   YA  NJE  WA TAIFA HILO  KUWA   ANAPOTEZA  MUDA  WAKE  KUFANYA  MAZUNGUMZO NA KOREA YA KASKAZINI Reviewed by safina radio on October 02, 2017 Rating: 5

No comments