UFARANSA KUWAPA HIFADHI WAKIMBIZI ELFU KUMI
TAREHE 10-10-2017
Serikali
ya Ufaransa inapanga kuwaruhusu jumla ya wakimbizi elfu kumi kutoka nchi kadhaa
zisizo za Ulaya kuingia nchini humo kihalali katika
kipindi cha miaka miwili ijayo kama sehemu ya mpango ya kuwapa makazi
wakimbizi.
Rais
wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema watashirikiana na ofisi ya kamishna mkuu wa
Umoja wa Mataifa kuhusu kuwaruhusu
wakimbizi kutoka Uturuki, Jordan, Niger na Chad kuingia Ufaransa.
Halmashauri
kuu ya Umoja wa Ulaya iliwasilisha mpango mpya wa kuwapa wakimbizi hifadhi wiki
mbili zilizopita ambao utaruhusuu wakimbizi elfu hamsini kupata hifadhi Ulaya
katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Umoja wa Ulaya umesema mpango huo mpya
utawalenga watu walio katika mazingira hatari kutoka Libya, Misri, Niger,
Sudan, Chad na Ethiopia mbali na wanaotoka Uturuki na kanda ya Mashariki ya
Kati.
UFARANSA KUWAPA HIFADHI WAKIMBIZI ELFU KUMI
Reviewed by safina radio
on
October 10, 2017
Rating:

No comments