SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ASASI BINAFSI ZINAZOHUSIKA NA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
TAREHE 25-10-2017
Serikali
imeahidi kutatua changamoto zinazozikumba asasi binafsi zinazohusika na
uhifadhi wa wanyama pori ili kuleta maendeleo baina ya pande zote mbili .
Hayo
yamesemwa na Katibu mkuu wa wizara ya mali asili na utalii Meja jenerali Gaudence Milanzi jijini Dar es
salaam baada ya kushiriki kikao na asasi binafsi ishirini na tano zinazohusika
na uhifadhi wa wanyama pori nchini.
Kwa
upande wake mkurugenzi idara ya wanyama
pori wizara ya mali asili na utalii, Profesa Alexanda Songorwa amesema kuwa
wizara hiyo ina matarajio ya kusonga mbele katika kuhifadhi wanyama pori.
Hata
hivyo katika kikao hicho wadau wa uhifadhi wa wanyama pori wamehimizwa
kushiriki vyema katika shughuli za kijamii kwenye maeneo waliyowekeza ikiwemo
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili jamii inayowazunguka..
SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI ASASI BINAFSI ZINAZOHUSIKA NA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
Reviewed by safina radio
on
October 25, 2017
Rating:

No comments