Ujerumani yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018
TAREHE 06-10-2017
Sebastian Rudy alifunga bao
dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili baadaye, naye Joshua Kimmich
akafunga la tatu mechi ikikaribia kumalizika.
Josh Magennis alifungia
Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala
salama.
Ujerumani wamefuzu wakiwa
viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia bado na matumaini ya
kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu Novemba.
Vijana hao wa Michael O'Neill
watamaliza mechi zao Kundi C nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa
miongoni mwa timu nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa
ya kufuzu.
Ujerumani yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018
Reviewed by safina radio
on
October 06, 2017
Rating:

No comments