TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA UTALII

TAREHE 18-10-2017



Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangala amesema kuwa Tanzania na nchi ya Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya utalii kwa nchi hizo mbili, ambapo watashirikiana katika mwingiliano wa watalii watakao kuwa wakitokea moja kwa moja Oman  kuja Tanzania.

Dk. Kigwangala amesema kuwa mpango huo ni pamoja na watalii wanaokwenda Oman na kutaka kuja nchi za Afrika wataelekezwa  moja kwa moja Tanzania kwa kuwa nchi hiyo ina watalii wengi.


Awali Dk. Kigwangala ametembelea meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mh. Qaboos Bin Said iliyofika  juzi  katika Bandari ya Dar es salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya serikali ya Oman na Tanzania.
TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA UTALII TANZANIA  NA  OMAN   KUSHIRIKIANA   KATIKA  SEKTA   YA   UTALII Reviewed by safina radio on October 18, 2017 Rating: 5

No comments