MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA KUTOKA SUMBAWANGA HADI KASANGA ATAKIWA KUKAMILISHA KWA WAKATI

TAREHE 17-10-2017


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemwangiza Meneja  wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Rukwa kuhakikisha kuwa Mkandarasi anayejenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Sumbawanga hadi bandari ndogo ya Kasanga wilayani Kalambwe inakamilika kwa wakati.

Prf. Mbarawa ametoa agiza hilo Mkoani Rukwa wakati akikagua ujenzi wa barabara za lami Mkoani humo na kusisitiza kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita mia moja na kumi inatakiwa kukamilika kabla ya mwezi septemba, 2018.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoani Rukwa Msuka Mkina amesema mkandarasi wa barabara hiyo China Rellway Cooperation ameahidi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.


Hata hivyo kukamilika kwa barabara hiyo kunatajwa kuwa kichocheo kikubwa cha kufungua milango ya kibiashara baina ya Tanzania na nchi za jirani.
MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA KUTOKA SUMBAWANGA HADI KASANGA ATAKIWA KUKAMILISHA KWA WAKATI MKANDARASI   ANAYEJENGA    BARABARA  KUTOKA  SUMBAWANGA   HADI  KASANGA  ATAKIWA  KUKAMILISHA   KWA  WAKATI Reviewed by safina radio on October 17, 2017 Rating: 5

No comments