MGOMO WATISHIA KUKWAMISHA KAZI KATIKA JIMBO LA KATALONIA
TAREHE 03-10-2017
Mgomo mkubwa unatishia kukwamisha
shughuli katika sehemu kubwa za Catalonia nchini Uhispania kufuatia kura ya
maoni yenye utata.
Mgomo huo ulioitishwa na vyama vya
wafanyakazi huko Catalonia, unalalamikia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu
ulioshuhudiwa wakati wa kura ya maoni siku ya Jumapili.
Uhispania imeitaja kura hiyo ya
maoni kuwa iliyo kinyume na sheria huku raia waliopiga kura hiyo wakitajwa kuwa
ni zaidi ya milioni 2.2 ambapo mimia yao walijeruhiwa wakati polisi wa
Uhispania wakijaribu kuzuia zoezi hilo kutoendelea.
Baadhi ya maafisa walioamrishwa
kuwazuia watu wasipige kura walionekana wakifyatua risasi za mipira, wakivamia
vituo vya kupigia kura na kuwavuta wanawake nywele zao huk maafisa wa afya huko
Catalonia wakisema kuwa Polisi 3 walijerihiwa siku ya Jumapili.
Habari zinaeleza kuwa mgomo
huo wa leo Jumanne utavuruga shushuli za usafiri wa umma, shule na zahahati
huko Catalonia ambapo Klabu maarufu cha mpira wa miguu cha Barcelona pia kikitarajiwa
kugoma, licha ya kuwa hawachezi mechi huku vyuo vya umma na makavazi nayo
yakitarajiwa kugoma.
MGOMO WATISHIA KUKWAMISHA KAZI KATIKA JIMBO LA KATALONIA
Reviewed by safina radio
on
October 03, 2017
Rating:

No comments