VIONGOZI WAWILI WAFUNGWA NCHINI UHISPANIA KWA UCHOCHEZI
TAREHE 17-10-2017
Jaji wa
mahakama moja nchini Uhispania ameamuru kufungwa kwa viongozi wawili wa
vuguvugu linalounga mkono uhuru wa jimbo la Catalonia kwa mashitaka ya
uchochezi.
Viongozi hao wanatuhumiwa kuwataka wafuasi wao
kuwazuia polisi wasifanye uvamizi wakati wa kura ya maoni mwanzoni mwa mwezi
huu, ambayo viongozi wa Catalonia wanasema takribani asimilia 90 ya wapiga kura
waliunga mkono jimbo hilo kujitangazia uhuru kutoka Uhispania.
Jaji
huyo amewatia hatiani viongozi hao kwa kutumia mitandao ya kijamii kuitisha
maandamano.
Waziri
Mkuu wa Uhispania, Mariano Rajoy, alimpa Rais Carles Puigdemont hadi kesho
kutwa Alhamisi awe ameshaweka bayana endapo ametangaza uhuru wa jimbo hilo
tajiri la kaskazini.
VIONGOZI WAWILI WAFUNGWA NCHINI UHISPANIA KWA UCHOCHEZI
Reviewed by safina radio
on
October 17, 2017
Rating:

No comments