KWA MUJIBU TAFITI ZILIZOFANYWA ZIMEONYESHA KUWA TAKRIBANI MIAKA 15 IJAYO KUTAKUWA NA UKOSEFU WA NYAMA NYEKUNDU

TAREHE 26-10-2017


Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi  Mh Abdallah Ulega amesema kuwa tafiti zilizofanywa na wataalam wa mifugo zinaonyesha kuwa  takribani miaka 15 ijayo kutakuwa na ukosefu wa nyama nyekundu kutokana na kutofanyika kwa mikakati mahususi ya uwekezaji katika mifugo na uvuvi. 

Mh Ulega ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wataalamu wa mifugo unaoendelea jijini Arusha ambao umelenga kubadilishana mawazo na uzoefu kwa wataalamu hasa kwenye shughuli mbalimbali wanazozifanya katika sekta ya mifugo na uvuvi. 

Amesema kuwa nchini Tanzania  watu hufuga mifugo yao na kuizalisha kwa njia za kienyeji ambazo haziwaletei manufaa hivyo amewataka wafugaji kufuga mifugo michache ambayo itaweza kuwaletea faida wao binafsi na taifa kwa ujumla. 

Aidha ameongeza kuwa mifugo na uzalishaji nyama iwe sehemu ya mapambano ya kuwa na Tanzania ya viwanda kwa kuwa na nyama za uhakika katika viwanda ili kuweza kutosheleza soko la ndani na kupunguza gharama za manunuzi ambazo baadhi ya wananchi hushindwa kununua nyama kutokana na ukubwa wa gharama. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa mifugo Tanzania Dkt. Daniel Komuyangiro amesema kuwa kupitia mkakati wa Tanzania of máster plan serikali itaweza kuwekeza katika uzalishaji wa nyama nyeupe ambao utawasaidia wafugaji kuondokana na umaskini sambamba na kupunguza mahitaji ya nyama nchini. 
KWA MUJIBU TAFITI ZILIZOFANYWA ZIMEONYESHA KUWA TAKRIBANI MIAKA 15 IJAYO KUTAKUWA NA UKOSEFU WA NYAMA NYEKUNDU KWA  MUJIBU TAFITI ZILIZOFANYWA  ZIMEONYESHA  KUWA TAKRIBANI MIAKA 15 IJAYO KUTAKUWA NA UKOSEFU WA NYAMA NYEKUNDU Reviewed by safina radio on October 26, 2017 Rating: 5

No comments