JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAPOKEA MSAADA WA SARUJI
TAREHE 10-10-2017
Jeshi la polisi Mkoani Arusha limepokea jumla ya mifuko elfu moja na mia tatu ya saruji kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa makazi mapya ya nyumba za polisi zilizoteketea kwa moto hivi karibuni.
![]() |
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA CHARLES MKUMBO |
Jeshi la polisi Mkoani Arusha limepokea jumla ya mifuko elfu moja na mia tatu ya saruji kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa makazi mapya ya nyumba za polisi zilizoteketea kwa moto hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada
huo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo amewashukuru wadau
hao kwa kujitoa kusaidia ujenzi huo.
Kamanda Mkumbo amesema msaada huo utawawezesha kwa kiwango
kikubwa katika kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi ya familia 13 ambao pia
walipoteza mali zao.
Aidha ameyaomba makampuni mengine kuiga mfano huo wa kujitoa kwa
moyo katika kusaidia ujenzi huo pamoja na jamii nyingine zenye uhitaji ili
kuweza kuleta maendeleo katika Taifa.
Hata hivyo moto ulioteketeza nyumba hizo za askari katika
eneo la Sekei jijini Arusha ulitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu,ambapo siku moja
baada ya janga hilo rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli
alitoa kiasi cha shilingi milioni mia mbili sitini kwa ajili ya kusaidia ujenzi
wa majengo hayo.
JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LAPOKEA MSAADA WA SARUJI
Reviewed by safina radio
on
October 10, 2017
Rating:

No comments