VIONGOZI WA AFRIKA MAGHARIBI WAMETOA MAONI YAO JUU YA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI TOGO
TAREHE26-10-2017
Viongozi wa Afrika Magharibi wametoa maoni yao ya kwanza baada ya miezi
miwili ya vurugu mbaya zinazoendelea nchini Togo.
Viongozi hao wamemtaka rais wa Togo Faure Gnassingbe na upande wa upinzani
kufanya mazungumzo ili kusuluhisha mgogoro wa kisiasa uliopo nchini humo.
Ufaransa pia imetoa mwito wa kufanyika majadiliano ya haraka baina ya pande
hizo mbili katika nchi iliyokuwa zamani ni koloni lake na kusema kuwa ina
wasiwasi kutokana na ripoti kwamba wapiganaji wa kiraia wanafanya kazi pamoja
na vikosi vya usalama.
Takriban watu16 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika maandamano ya
kuipinga serikali.
Rais wa Ivory Coast Alassane
Ouattara amesema yeye na wenzake kutoka Nigeria, Niger na Ghana walikutana siku
ya Jumanne na Rais wa Togo Faure Gnassingbe kujadili juu ya suala hilo.
VIONGOZI WA AFRIKA MAGHARIBI WAMETOA MAONI YAO JUU YA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI TOGO
Reviewed by safina radio
on
October 26, 2017
Rating:

No comments