JUHUDI ZA KIDIPLOMASIA KUENDELEA ILI KUTATUA MGOGORO WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI
TAREHE 16-10-201
![]() |
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI REX TILLERSON. |
Waziri wa Mambo wa Nje wa Marekani,
Rex Tillerson, amesema kuwa juhudi za kidiplomasia kuutatua mzozo wa Korea
Kaskazini zitaendelea kabla nchi hiyo haijachukua
hatua za kijeshi.
Kauli ya Bw Tillerson
inakuja hata baada ya Rais Donald Trump kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter
wiki chache zilizopita, kwamba waziri wake huyo anapoteza muda kujadiliana na
kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jung-Un, aliyemwita mtu wa maroketi.
Akizungumza kwenye kipindi cha State
of the Union cha televisheni ya CNN hivi leo, Tillerson amesema huenda Trump
anataka kuweka wazi kwa Kim Jung-Un kwamba upo mpango wa kijeshi kama
diplomasia ikishindwa, lakini sio kwamba Marekani imeachana na juhudi hizo.
Hata hivyo mgongano huo wa kauli
kutoka ngazi za juu katika serikali ya Trump umezua wasiwasi juu ya uwezekano
wa kutopigwa hesabu vyema kwenye mzozo kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
JUHUDI ZA KIDIPLOMASIA KUENDELEA ILI KUTATUA MGOGORO WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI
Reviewed by safina radio
on
October 16, 2017
Rating:

No comments