WAZAZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA WAALIMU.
TAREHE 04-10-2017
Wazazi nchini wametakiwa kushirikiana kwa
karibu na waalimu katika kuwahimiza na kuwalekeza watoto wao kusoma kwa bidii.
Wito huo umetolewa na Afisa elimu wa Shule za Msingi Halmashauri
ya Mji wa Babati, Bi. Doroth Mwandila wakati akizungumza na wazazi na wanafunzi wa halmashauri hiyo juu ya umuhimu wa kuwa karibu na watoto wa shule ili kuongeza ufaulu na maadili
katika jamii.
Mwandila amesema ili kufikia azma ya maendeleo ya viwanda nchini
yanayohamasishwa na Serikali ya awamu ya tano ipo haja ya wazazi kushirikiana
na walimu ili kuzalisha kizazi kitakacho kuwa na elimu na wajibu wa kujituma.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya
Msingi Deira iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara Daniel Gaitu amesema
wameitikia wito wa kuwafundisha wanafunzi masomo ya sayansi ili kuzalisha
wataalam watakaotumika katika miradi mbalimbali.
Naye Mwanafunzi Edson Eliudi wa Shule ya
Msingi Deira aliyeongoza nafasi ya kwanza kwenye mitihani ya majaribio
iliyohusisha Shule 37 zilizopo Halmashauri ya Mji wa Babati amesema kuwa siri
ya mafanikio yake ilitokana na wazazi wake kumfuatilia kimasomo na kuwa
karibu naye pamoja na walimu.
WAZAZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA WAALIMU.
Reviewed by safina radio
on
October 04, 2017
Rating:

No comments