WAZIRI ANGELA KAIRUKI AITAKA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUIPATIA SERIKALI WATU WENYE SIFA

TAREHE  06-10-2017
WAZIRI  ANGELA  KAIRUKI


Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora Mh Angela Kairuki ameitaka bodi ya sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma kuipatia serikali rasilimali watu wenye sifa stahiki weledi na uwezo wa kuwezesha serikali kutimiza malengo yake.

Mh Kairuki ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya tatu ya sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma jijini Dar-es-salaam,ambapo amesema kuwa dhamira ya serikali ni kujenga utamaduni wa kutaka watu kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Amesema kuwa kila mmoja anafahamu azma ya serikali ya kutaka kuingia katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda kwa hiyo bodi hiyo ina majukumu makubwa sana kuliwezesha taifa kupata rasilimali watu ambao wana weledi,uadilifu na uzalendo wa kutosha katika kulitumikia taifa.


Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo Bi Rose Lugembe amesema kuwa watahakikisha wanazingatia sheria kanuni na taratibu ili kuwezesha serikali kupata watumishi watakaowezesha kupeleka gurudumu  la maendeleo mbele.
WAZIRI ANGELA KAIRUKI AITAKA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUIPATIA SERIKALI WATU WENYE SIFA WAZIRI   ANGELA   KAIRUKI   AITAKA   SEKRETARIETI   YA  AJIRA  KATIKA   UTUMISHI  WA  UMMA  KUIPATIA  SERIKALI   WATU   WENYE  SIFA Reviewed by safina radio on October 06, 2017 Rating: 5

No comments