MGOMBEA URAIS NCHINI LIBERIA NA MWANASOKA WA ZAMANI WA TAIFA HILO GEORGE WEAH AKIRI KUWA NA MAWASILIANO NA RAIS WA ZAMANI CHARLES TAYLOR
TAREHE 06010-2017
![]() |
GEORGE WEAH |
Mmoja
wa wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Liberia na nyota wa soka George
Weah amekiri kuwa na mawasiliano na kiongozi wa zamani wa taifa hilo Charles
Taylor.
Bw Taylor anatumikia
kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makossa uhalifu wa kivita baada
ya kuhukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa.
Bw Weah amesema kuwa
alipokea simu kutoka kwa mbabe huyo wa kivita, lakini akakanusha kwamba Charles
Taylor ana ushawishi wa mambo nchini humo.
Wiki iliyopita, Bunge la
Congress nchini Marekani liliidhinisha azimio la kushutumu juhudi zozote za
mbabe huyo wa zamani wa kivita za kujaribu kuwa na ushawishi kwenye uchaguzi
nchini Liberia kutoka gerezani.
Hata hivyo George Weah ni
mmoja wa wagombea 11 ambao wamejitokeza kutaka kumrithi Rais Ellen
Johnson-Sirleaf ambaye anastaafu.
MGOMBEA URAIS NCHINI LIBERIA NA MWANASOKA WA ZAMANI WA TAIFA HILO GEORGE WEAH AKIRI KUWA NA MAWASILIANO NA RAIS WA ZAMANI CHARLES TAYLOR
Reviewed by safina radio
on
October 06, 2017
Rating:

No comments