MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA AWATAKA WATAALAMU WA AFYA MATIBABU WALEMAVU
TAREHE 02-10-2017
Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Anna Mghwira
ameiagiza timu ya wataalamu wa afya mkoani humo kuhakikisha wanafuata watu
wenye ulemavu majumbani na kuwapatia huduma za matibabu ili kuwaepusha na
gharama za kufuata matibabu katika vituo vya afya.
Mghwira ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kutembelea familia moja yenye watoto watano walemavu na wenye mtindio wa ubongo iliyopo chome wilayani Same mkoani Kilimanjaro,ambapo ziara hiyo iliratibiwa na mmiliki wa shule ya Upendo Friends Bi Isabela Mwampamba kwa lengo la kutoa msaada katika familia hiyo.
Amesema kuwa kufuatia familia hiyo kuwa na watoto watano wenye ulemavu wasio na uwezo wataalam wa afya wanapaswa kutembelea makundi yote ya watu wenye ulemavu majumbani na kuhakikisha wanawapatia matibabu ya afya wakiwa nyumbani kwani wengi wa walemavu wanashindwa kufikishwa vituo vya afya kutokana na mazingira kutoruhusu.
Nae mmiliki wa shule ya upendo friends Bi Isabela Mwampamba amesema kuwa aliguswa kufika katika familia hiyo ili kutoa msaada wa chakula kumtia moyo mama mzazi wa walemavu hao ambaye ndie amekuwa akiwahudumia watoto hao peke yake.
Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo ya fedha na mchele mama mzazi wa walemavu hao Bi Nehenjiwa Mgonja amesema kuwa msaada huo umempa matumaini na faraja kwake ambapo alimshukuru mfadhili huyo huku akitoa kilio chake kwa serikali kuipatia familia hiyo umeme kwani ni moja ya changamoto inayowakabili walemavu hao haswa nyakati za usiku .
![]() |
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA |

Reviewed by safina radio
on
October 02, 2017
Rating:

No comments