KIONGOZI WA KATALONIA AAPA KUTANGAZA UHURU WA JIMBO HILO
TAREHE 19-10-2017
![]() |
CARLES PUIGDEMONT KUSHOTO NA WAZIRI MKUU WA UHISPANIA KULIA MARIANO RAJOY |
Kiongozi
wa Catalonia ameapa kwamba atatangaza uhuru, endapo serikali ya Uhispania
italazimisha utawala wa moja kwa moja kutoka mjini Madrid.
Serikali kuu mjini Madrid imemtaka (Kales
pugidemont) Carles Puigdemont
kuachana na mipango ya kujitenga aliyoitangaza wiki iliyopita .
Mzozo wa kisiasa umezidi kupamba moto tangu
kufanyika kwa kura ya maoni ya tarehe 1 Oktoba, ambayo zaidi ya asilimia 90 ya
Wakatalonia waliamua kuunda taifa lao, na ambayo Uhispania inasema haikuwa
halali.
Hata
hivyo hatua ya kuiondolea Catalonia mamlaka yake ya ndani iliyonayo inahitaji
kura kwenye bunge la Uhispania, ambako chama cha Waziri Mkuu Mariano Rajoy kina wingi wa kutosha.
KIONGOZI WA KATALONIA AAPA KUTANGAZA UHURU WA JIMBO HILO
Reviewed by safina radio
on
October 19, 2017
Rating:

No comments