WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH. MWIGULU NCHEMBA AMEWASHUKURU WADAU WALIOJITOLEA KUJENGA NYUMBA ZA POLISI ZILIZOUNGUA MKOANI ARUSHA

TAREHE 17-10-2017

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu Nchemba amewashukuru wadau mbalimbali waliojitolea kujenga nyumba za askari polisi zilizoungua hivi karibuni mkoani Arusha.

Akizungumza na wanahabari  Mara baada ya kukagua  Ujenzi wa nyumba hizo  mapema Leo  Nchemba amesema kuwa wadau waliojitolea katika Ujenzi huo  wamefanya vyema ili kuharakisha ukamilishaji wa nyumba hizo.

Amesema Rais wa nchi Mhe John Pombe Magufuli anatambua umuhimu wa jeshi hilo ndio maana alitoa  pesa ili kuhakikisha nyumba hizo zinajengwa kwa haraka ambapo pia  amemtaka mkuu wa Wilaya ya Arusha kumweleza mkuu wa mkoa  kuwa wanapaswa kupanga namna ya kukutana ili kuangalia katika wizara ya mambo ya ndani jinsi ambavyo wanakwenda  kumalizia Ujenzi wa nyumba hizo.

Naye Kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amemshukuru rais pamoja na wadau mbalimbali kwa namna walivyojitolea kuhakikisha askari wanarudi kwenye makazi yao haraka iwezekanavyo kutokana na majengo hayo kujengwa kwa haraka.

Hata hivyo kwa upande wa Mmoja wa wadau wanaojitolea katika Ujenzi huo Hussain Gonga ambaye ni Mkurugenzi wa Tanzanite One amesema wameamua kujitoa katika kusaidia Ujenzi huo kutokana nakutambua umuhimu wa jeshi  hilo ambapo  amesema Usalama ndio kila kitu na wanaolinda Usalama ni askari  hivyo ni muhimu kukaa katika Mazingira bora.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH. MWIGULU NCHEMBA AMEWASHUKURU WADAU WALIOJITOLEA KUJENGA NYUMBA ZA POLISI ZILIZOUNGUA MKOANI ARUSHA WAZIRI WA MAMBO   YA NDANI  MH. MWIGULU  NCHEMBA AMEWASHUKURU  WADAU  WALIOJITOLEA  KUJENGA  NYUMBA  ZA POLISI  ZILIZOUNGUA   MKOANI  ARUSHA Reviewed by safina radio on October 17, 2017 Rating: 5

No comments