RAIS WA TANZANIA MH.. JOHN MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI LEO
TAREHE 09-10-2017
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John
Magufuli leo amewaapisha mawaziri na manaibu waziri baada ya kufanya mabadiliko
katika baraza lake la mawaziri mwishoni mwa wiki.
Hafla ya kuwaapisha mawaziri hao imefanyika ikulu
jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo makamu wa
rais Mh Samia Suluhu Hassan,waziri mkuu Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa,Spika wa
Bunge Mh Job Ndugai,jaji mkuu wa Tanzania Mh Ibrahim Juma,makatibu wakuu,na
viongozi wengine wa serikali na vyama vya siasa.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa mawaziri hao
spika wa bunge Mh Job Ndugai amewapongeza wale wote walioteuliwa kushika nafasi
hizo na kuwataka kwenda kufanya kazi kwa bidii kama walivyoaminiwa na Mh Rais, huku
jaji mkuu Ibrahim Juma akiwataka mawaziri hao kufanya kazi
kwa mujibu wa sheria
ili pasije pakatokea mwingilano wa majukumu.
Naye Mh George Mkuchika ambaye ameapishwa kuwa
waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora amesema kuwa,katika majukumu
yake atahakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa bidii na kuondoa urasimu
katika maeneo ya kazi kwa kuzingatia
sheria na utawala bora.
Hata hivyo katika hafla hiyo jumla ya mawaziri walioapishwa
ni 7 manaibu waziri 14 na katibu wa bunge mmoja ambaye ni Bw Steven Kigaigai.
RAIS WA TANZANIA MH.. JOHN MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI LEO
Reviewed by safina radio
on
October 09, 2017
Rating:

No comments