VITUO VYA AFYA VIMEONYWA KUTOKUGHUSHI NYARAKA ZA MADAI

tarehe 06-10-2017


Vituo vya afya Mkoani Manyara vimeonywa kutokughushi nyaraka za madai ya kupatiwa msaada kutoka mfuko wa bima ya afya ulioboreshwa [ICHF] na badala yake vifuate sheria, kanuni na utaratibu wa mfuko huo.

Wito huo umetolewa katika mkutano  mkuu wa wadau wa afya na Mkurugenzi  wa mfuko wa bima ya afya ulioboreshwa hapa nchini Bw. Hance Mwankenja,ambapo amesema kuwa mfuko huo unahudumia   Halmashauri saba za Mkoa wa Manyara  zenye jumla ya vituo 202 ambavyo  ndani yake kuna hospitali,zahanati na vituo vya afya.

Bw. Mwankenja amesema kuwa kumekuwa na tabia ya vituo vinavyohudumiwa na mfuko huo kughushi nyaraka za madai kwa lengo la kujipatia manufaa zaidi,hivyo amewaonya wamiliki wa vituo wenye tabia kama hiyo kuacha mara moja la sivyo vituo hivyo vitafungiwa.

Aidha amesema  kuwa kuna baadhi ya changamoto zinazowakabili katika huduma wazozitoa  ikiwemo kutokuwepo kwa maabara katika vituo vingi vya serikali hali inayopelekea wananchi kuhoji ukamilifu wa
matibabu  huku changamoto nyingine ikiwa ni  vituo vingi
vinavyomilikiwa na serikali havina watumishi na kama wapo wanakuwa
hawana sifa  zinazohitajika kukidhi mahitaji  ya walengwa.

Hata  hivyo ili kuhakikisha mfuko huo unaendelea kuboresha huduma
zake  umejipanga  kusajili maduka ya dawa vijijini  ili kutatua

changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwa ni pamoja na  kusajili maduka ya dawa muhimu .
VITUO VYA AFYA VIMEONYWA KUTOKUGHUSHI NYARAKA ZA MADAI VITUO   VYA   AFYA   VIMEONYWA   KUTOKUGHUSHI  NYARAKA  ZA MADAI Reviewed by safina radio on October 06, 2017 Rating: 5

No comments