RAIS WA BARAZA LA ULAYA DONALD TUSK AELEZEA MASHARTI YA UINGEREZA KUJITOA KATIKA UMOJA WA ULAYA

TAREHE 25-10-2017

Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, ameyaelezea mazungumzo kuhusu masharti ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, mchakato unaojulikana kama Brexit, kuwa magumu na mtihani mkubwa kwa umoja huo.
Akizungumza leo wakati wa mjadala kwenye bunge la Umoja wa Ulaya,Tusk amesema kwa mazungumzo ya Brexit, wamefanikiwa kujenga na kudumisha umoja miongoni mwa nchi wanachama 27, lakini kilicho mbele yao bado ni kigumu na mtihani mkubwa.
 Pande zote hizo zimeshakutana mara tano kukubaliana kuhusu masharti ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, na mazungumzo mengine yamepangwa kufanyika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Wakati huo huo, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker, amesema umoja huo bado unafanya kazi ili kufikiwa makubaliano ''yenye haki'' na Uingereza na kwamba kutofikiwa kwa makubaliano, sio dhana yao ya kufanya kazi.
RAIS WA BARAZA LA ULAYA DONALD TUSK AELEZEA MASHARTI YA UINGEREZA KUJITOA KATIKA UMOJA WA ULAYA RAIS WA BARAZA LA ULAYA  DONALD TUSK  AELEZEA MASHARTI YA UINGEREZA  KUJITOA KATIKA UMOJA WA ULAYA Reviewed by safina radio on October 25, 2017 Rating: 5

No comments