ODINGA ATANGAZA KUJIONDOA KWENYE UCHAGUZI

TAREHE 11-10-2017


Kinara wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Raila Odinga ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarahe 26 mwezi huu, akihoji maafisa wa tume ya uchaguzi kwamba wameshindwa kufanya mageuzi yanayohitajika.

Raila amesema baada ya kutafakari msimamo wao kuhusiana na uchaguzi ujao, na kwa kuzingatia maslahi ya Wakenya, kanda na ulimwengu kwa jumla wanaamini ni jambo la busara kujiondoa kama mgombea urais katika uchaguzi huo.

Uamuzi huo wa Raila unakuja wakati ambapo mswada uliowasilishwa bungeni na chama tawala cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta ukinuuia kuifanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ili kuepusha mzozo wa kisiasa iwapo kiongozi wa muungano wa NASA Raila Odinga atajiondoa katika uchaguzi mpya wa urais katika dakika ya mwisho.

Marekebisho hayo yataruhusu mgombea anayesalia kuapishwa moja kwa moja.Mahakama ya juu nchini Kenya iliamuru uchaguzi mpya wa urais ufanywe baada ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa rais wa Agosti nane kwasababu ulikumbwa na dosari
ODINGA ATANGAZA KUJIONDOA KWENYE UCHAGUZI ODINGA ATANGAZA KUJIONDOA KWENYE UCHAGUZI Reviewed by safina radio on October 11, 2017 Rating: 5

No comments