ZAIDI YA NYUMBA MIA MOJA ZAARIBIWA VIBAYA KUTOKANA NA MVUA MKOANI KATAVI
13-10-2017
Zaidi ya Kaya mia moja
katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi hazina makazi baada ya mvua kubwa
iliyoambatana na upepo mkali na kuezua paa na kubomoa nyumba zao.
Mvua hizo zilizonyesha
kwa muda wa siku mbili zimesababisha kujeruhiwa kwa wakazi watatu wa Manispaa
hiyo.
Kata zilizoathirika na
upepo huo ni Kazima,Kasese na Nsemulwa ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Rafael Mhuga ametembelea maeneo hayo
kwa lengo la kujionea uharibifu uliotoke.
Akiwa katika eneo hilo,
Meja Jenerali Mstaafu Mhuga amebaini kuwapo kwa ujenzi usiozingatia maelekezo
ya wataalamu wa Mipango Miji na hivyo kuwa chanzo cha kuharibika kwa nyumba
hizo .
ZAIDI YA NYUMBA MIA MOJA ZAARIBIWA VIBAYA KUTOKANA NA MVUA MKOANI KATAVI
Reviewed by safina radio
on
October 13, 2017
Rating:

No comments