ODINGA AITISHA MAANDAMANO KUSHINIKIZA MAGEUZI KATIKA TUME YA UCHAGUZI IEBC
TAREHE 29-09-2017
![]() |
KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA RAILA ODINGA |
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga,
ametangaza jana kuwa ataitisha maandamano kushinikiza mageuzi ndani ya tume ya
uchaguzi na kukizuwia chama tawala kuondoa kinga dhidi ya udanganyifu kuelekea
uchaguzi mpya wa rais.
Odinga
ameitisha maandamano ya nchi nzima wiki ijayo, baada ya mazungumzo kuvunjika
jana kati ya tume ya uchauguzi, chama tawala cha Jubilee, na wawakilishi wake,
juu ya namna ya kufanya uchaguzi mpya wa rais.
Tume ya uchaguzi IEBC ilitangaza tarehe 26 Oktoba
kuwa siku ya uchaguzi mpya, baada ya mahakama ya juu kabisa nchini humo
kubatilisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kutokana na kukosekana kwa uhakiki
wa matokeo.
Odinga
anasema wadukuzi waliingilia mitambo ya kurusha matokeo ya tume ya uchaguzi na
kubadilisha matokeo.
ODINGA AITISHA MAANDAMANO KUSHINIKIZA MAGEUZI KATIKA TUME YA UCHAGUZI IEBC
Reviewed by safina radio
on
September 29, 2017
Rating:

No comments