BUNGE LA TUNISIA LAPITISHA SHERIA TATA ILI KUTOA MSAMAHA KWA WATU WANAOHUSISHWA NA MAKOSA YA RUSHWA






WABUNGE WA TUNISIA WAKIWA KWENYE KIKAO


Bunge la Tunisia limepitisha sheria tata inayolenga kutoa msamaha kwa maelfu ya watu nchini humo wanaohusishwa na rushwa, chini ya utawala wa kidikteta kabla ya vuguvugu la mapinduzi ya umma.

Baadhi ya watu waliandamana nje ya bunge hilo kupinga hatua hiyo wakisema wanahofia kuirudisha Tunisia katika enzi za kabla ya vuguvugu la mabadiliko.

Baada ya mjadala wa hasira na kutoka nje kwa wabunge wa upinzani, sheria hiyo ilipitishwa kwa kura 117 zilizounga mkono huku kura tisa zikipinga.

Rais wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 90 anasema sheria hiyo ya maridhiano ya kiuchumi itaboresha mazingra ya uwekezaji na kuiwezesha nchi hiyo kupiga hatua.


Msamaha kamili chini ya sheria hiyo utawahusu wale waliotekeleza amri kutoka kwa viongozi mafisadi lakini ambao hawakunufaika binafsi kutokana na hatua hizo walizochukua huku wale waliojipatia fedha kwa njia ya rushwa watalazimika kurejesha fedha hizo pamoja na faini ili kuepukana na kushitakiwa.












BUNGE LA TUNISIA LAPITISHA SHERIA TATA ILI KUTOA MSAMAHA KWA WATU WANAOHUSISHWA NA MAKOSA YA RUSHWA BUNGE LA TUNISIA LAPITISHA SHERIA TATA  ILI KUTOA MSAMAHA  KWA WATU WANAOHUSISHWA NA MAKOSA YA RUSHWA Reviewed by safina radio on September 14, 2017 Rating: 5

No comments