HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG MKOANI MANYARA IMEFANIKIWA KUTATUA MGOGORO KATI YAKE NA WIZARA YA NISHATI MADINI .


TAREHE 19-09-2017


KAMISHINA MSAIDIZI WIZARA YA NISHATI NA MDINI KANDA YA KASKAZINI  BW. ADAM JUMA
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ iliyopo mkoani Manyara imefanikiwa kutatua mgogoro uliokuwa ukiendelea kati yao na  wizara ya nishati na madini  kanda ya kasikazini uliokuwa ukihusiana na utozwaji wa ushuru katika  mgodi wa chumvi uliopo katika kata ya  Gendabi  wilayani humo.

Akizungumza katika mkutano na wakazi wa  vijiji vya Gendabi,Sebasi,Hargushay na Sarjanda  vyote vikiwa vinaunda kata ya Gendabi Kamishina msaidizi wa  wizara ya nishati na  madini kanda ya kasikazini Bw.Adam Juma alieleza kuwa mgogoro huo ulitokana  na fedha zilizokuwa  zikitolewa na serikali  kwa ajili ya kusaidia vikundi vidogo vidogo vya uchimbaji wa madini  kwa ajili ya  kuwakwamua  na kuwapa ari ya  kufanya kazi.

Amesema kuwa jumla ya vikundi 59  vilivyosajiliwa  hapa nchini vimenufaika na fedha hizo za serikali huku mkoa Wa manyara ukijwa kuwa na vikundi 6 ambapo  kukindi  kimojawapo ni cha uchimbaji wa chumvi katika mgondi wa chumvi  wa Hargushay kinachofahamika kwa majina ya Hasami kinachochimba chumvi katika mgondi huo pamoja na kuuza.

Naye mkuu wa wilaya  ya Hanang’ Sarah Msafiri  amesema  chumvi inayozalishwa  katika mgondi huo imekuwa ikisafirishwa kwenda nchi za Rwanda,Burundi,Kenya  na Malawi  kwa ajili ya matumizi mabalimbali lakini mafanikio  ni kidogo ikilinganishwa na uchimbaji unaofanywa katika mgondi huo na hiyo ni kutokana na  kukosa usimamizi wa kukusanya mapato katika njia zilizosahihi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG MKOANI MANYARA IMEFANIKIWA KUTATUA MGOGORO KATI YAKE NA WIZARA YA NISHATI MADINI . HALMASHAURI  YA   WILAYA  YA    HANANG  MKOANI  MANYARA  IMEFANIKIWA  KUTATUA   MGOGORO  KATI  YAKE  NA  WIZARA   YA  NISHATI   MADINI  . Reviewed by safina radio on September 19, 2017 Rating: 5

No comments