IRAN YAPUUZIA HOTUBA YA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP




TAREHE 20-09-2017

RAIS DONALD TRUMP  WA MAREKANI

Iran imeipuuzia hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyoitoa katika Umoja wa Mataifa mjini New york na kuita kuwa ni hotuba yenye chuki.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mtandao wake wa Twitter ameiita hotuba hiyo ya Rais Trump kuwa ni ya zama za kati.

Rais wa Marekani ameituhumu serikali ya Iran kwamba ni utawala wa kiuaji na kupendekeza kuwa hata yaheshimu makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama.

Rais Trump alitishia pia kuiteketeza Korea kaskazini iwapo shughuli zake za kinyuklia zitaihatarisha Marekani au washirika wake.

Rais huyo wa Marekani katika hotuba yake hiyo ya Umoja wa Mataifa hakuacha pia kuitaja Venezuela. 
IRAN YAPUUZIA HOTUBA YA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP IRAN   YAPUUZIA    HOTUBA   YA   RAIS   WA   MAREKANI   DONALD   TRUMP Reviewed by safina radio on September 20, 2017 Rating: 5

No comments