ALSHABAAB WAMEISHAMBULIA KAMBI YA JESHI KATIKA MJI WA BARIRE NCHINI SOMALIA.

TAREHE 29-09-2017

WANAMGAMBO  WA ALSHABAAB
Nchi ya Somalia imesema kuwa wanamgambo wa Alshabaab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.

Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa majira ya alfajiri ambapo wakaazi wa maeneo hayo wanasema waliamshwa na sauti za milipuko miwili mikubwa.

Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa.

Hata hivyo maafisa wa serikali katika eneo hilo wamekana tuhuma hizo za Alshabaab, lakini wakakiri kwamba kumekuwa na shambulio.

Kambi hiyo ya jeshi mjini Barire katika eneo la Lower Shabelle ni mojawapo ya kambi zilizo bora na zenye vifaa vya hali ya juu vya kijeshi nchini Somalia
ALSHABAAB WAMEISHAMBULIA KAMBI YA JESHI KATIKA MJI WA BARIRE NCHINI SOMALIA. ALSHABAAB   WAMEISHAMBULIA   KAMBI  YA  JESHI  KATIKA  MJI   WA  BARIRE  NCHINI SOMALIA. Reviewed by safina radio on September 29, 2017 Rating: 5

No comments