MKANDARASI ANAYEJENGA DARAJA LA MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM AAGIZWA KUKAMILISHA MRADI HUO
TAREHE 26-09-2017
![]() |
WAZIRI WA UJENZI,MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO MH. MAKAME MBARAWA MNYAA |
Waziri
wa ujenzi,miundombinu na mawasiliano Mh Makame Mbarawa Mnyaa amemwagiza
mkandarasi anayejenga daraja la Mlalakuwa jijini Dar-es-salaam kukamilisha
mradi huo ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.
Mh
Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja
hilo,ambapo amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya upanuzi wa barabara ya Mwai
Kibaki Old Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 5.3 na umekamilika kwa asilimia 42
hadi sasa.
Kwa
upade wake mhandisi wa miradi ofisi ya meneja mkoa wa Dar-es-salaam Bw Julias
Ngusa amemwakikishia waziri Mbarawa kuwa mradi huo utakamilika katika kipindi
kilichopangwa licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa katika ujenzi huo.
Hata
hivyo daraja hilo lilianzwa kujengwa tarehe 25 Octoba mwaka wa 2016 na mpaka
sasa umekamilika kwa asilimia 42 katika kipindi cha miezi 10.
MKANDARASI ANAYEJENGA DARAJA LA MLALAKUWA JIJINI DAR ES SALAAM AAGIZWA KUKAMILISHA MRADI HUO
Reviewed by safina radio
on
September 26, 2017
Rating:

No comments