KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA, RAILA ODINGA AMETANGAZA KUWA MUUNGANO WA NASA UTASHINIKIZA MAGEUZI KATIKA TUME YA UCHAGUZI IEBC
TAREHE 18 -09-2017
![]() |
KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA RAILA ODINGA |
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa muungano wake wa NASA utaendesha kampeni nchi nzima kushinikiza kufanyika mageuzi katika tume ya uchaguzi, IEBC, akitaka maafisa wa tume hiyo kuondolewa.
Odinga
amesisitiza kuwa tume hiyo lazima ifanyiwe mageuzi kabla hajashiriki katika
uchaguzi wa marudio, huku Rais Kenyatta akisema tume hiyo haitakiwi
kubadilishwa.
Hata hivyo
licha ya mahakama ya juu nchini Kenya kugundua kuwepo kwa udanganyifu katika
uchaguzi huo, haikuwaondoa maafisa wa tume hiyo ambapo uchaguzi mkuu wa marudio
umepangwa kufanyika octoba 17 mwaka huu.
KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA, RAILA ODINGA AMETANGAZA KUWA MUUNGANO WA NASA UTASHINIKIZA MAGEUZI KATIKA TUME YA UCHAGUZI IEBC
Reviewed by safina radio
on
September 18, 2017
Rating:

No comments