RAIS MPYA WA ANGOLA KUAPISHWA LEO
TAREHE 26-09-2017
João Lourenço, aliyekuwa waziri wa ulinzi anachukuwa nafasi ya Jose Eduardo Dos Santos rais anayeondoka ambaye aliamua kuachia madaraka baada ya kuongoza nchini hiyo miaka 38.
Mwandishi mmoja wa habari nchini humo amesema kuwa watu wa Angola wanaunga mkono mabadiliko lakini huenda kusishuhudiwe mabadiliko makubwa kwa sababu Bw Lourenço amekuwa mwandani wa karibu wa chama tawala, ( Popular Liberation Movement of Angola MPLA) kwa miongo kadhaa.
Dos Santos atasalia kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye ana haki ya kumteua mkuu wa majeshi na polisi.
Chama cha MPLA kimeongoza Angola tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Mreno mwaka 1975
![]() |
RAIS MPYA WA ANGOLA JOAO LOURENCO |

Reviewed by safina radio
on
September 26, 2017
Rating:

No comments