WATU SABA WATIWA MBARONI NCHINI UGANDA






TAREHE 18-09-2017
WAANDAMANAJI  JIJIJNI KAMPALA

Takriban watu saba wametiwa nguvuni katika mji mkuu wa Uganda kampala, kufuatia maandamano ya kupinga mapendekezo ya mswada wa sheria unaoondoa kikomo cha umri wa mtu anayegombea urais.
Katiba ya sasa inasema kikomo cha umri wa urais ni miaka 75.
Mabadiliko ya katiba yatamruhusu rais Yoweri Museveni kugombea tena urais mwaka 2021.
Umri halisi wa rais Museveni haufahamiki, lakini mtandao mmoja wa kijamii unasema kuwa rais Yoweri Mseveni ana umri wa miaka 73

Wanaharakati vijana wa kundi linalojulikana kama-The Alternative, ambao waliandaa maandamano hayo, wanasema ofisi yao ilivamiwa jana na wanajeshi pamoja na polisi.
WATU SABA WATIWA MBARONI NCHINI UGANDA WATU SABA  WATIWA  MBARONI   NCHINI  UGANDA Reviewed by safina radio on September 18, 2017 Rating: 5

No comments