TAREHE 26-09-2017

Chama cha upinzani nchini Kenya NASA kimeitisha maandamano Jumanne hii nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi nchini humo.

Hatua hii ni ya kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa Augast 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini humo.

NASA umeeleza kwamba hautovamia makao ya tume ya IEBC kama ilivyotajwa awali kuwatimua kwa lazima maafisa hao, badala yake inasema maandamano hayo yatakuwa ya amani katika barabara za mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi hao wa tume ya uchaguzi.

Hilo ni mojawapo ya masharti iliyotoa NASA ndipo washiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.


Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wapinzani ambapo amesema ku watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi za raia wa nchi hiyo.
Reviewed by safina radio on September 26, 2017 Rating: 5

No comments