MKUU WA MKOA WA KAGERA MEJA MSTAAFU SALIM KIJUU AMETOA MUDA WA WIKI MOJA KWA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA HUO KUNYUNYIZIA DAWA ZA VIWATILIFU VYA MALARIA.







TAREHE 18-09-2017



MKUU WA MKOA WA KAGERA  MEJA MSTAAFU SALIM KIJUU

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja mstaafu Salim Kijuu ametoa muda wa wiki moja kwa halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha kuwa zinanyunyizia dawa za viwatilifu vya malaria zilizotolewa na serikali tangu mwezi Juni mwaka huu katika nyumba za wananchi wa wilaya hizo.

Brigedia Kijuu ametoa maagizo hayo katika kikao cha wadau kilicholenga kupanga mikakati ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani humo,ambapo maambukizi yamepanda kwa asilimia 35 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mkoani humo.

Amesema kuwa hategemei kuona dawa zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuulia mbu zinahifadhiwa katika magala kwa kuwa maeneo yanayotakiwa kunyunyiziwa dawa hizo yapo mengi ikiwemo madimbwi kwani lengo la serikali kutoa madawa hayo ni kuua mbu wanaowasumbua wananchi na kusababisha vifo hapa nchini.

Kwa upande wake mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Kagera Dr Julian Mgengi amesema kuwa licha ya juhudi mbalimbali kufanyika ikiwemo ugawaji wa vyandarua na unyunyiziaji wa dawa ya mkoko majumbani bado elimu inatakiwa kuendelea kutolewa ili wananchi wafahamu madhara zaidi yatokanayo na ugonjwa wa malaria.


Hata hivyo wilaya zitakazonufaika na zoezi hilo ni pamoja na Ngara,Misenyi na Bukoba vijijini ambazo kitakwimu inaonesha kuwa maambukizi ya malaria yamepungua kutokana na unyunyiziaji wa dawa uliofanyika mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
MKUU WA MKOA WA KAGERA MEJA MSTAAFU SALIM KIJUU AMETOA MUDA WA WIKI MOJA KWA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA HUO KUNYUNYIZIA DAWA ZA VIWATILIFU VYA MALARIA. MKUU  WA  MKOA  WA  KAGERA  MEJA  MSTAAFU  SALIM  KIJUU AMETOA  MUDA  WA  WIKI  MOJA  KWA  HALMASHAURI   ZOTE  ZA   MKOA   HUO   KUNYUNYIZIA   DAWA  ZA  VIWATILIFU   VYA   MALARIA. Reviewed by safina radio on September 18, 2017 Rating: 5

No comments