WAZIRI MKUU WA UHISPANIA MARIANO RAJOY ANATARAJIA KWENDA KATIKA JIMBO LINALOTAKA KUJITENGA LA CATALONIA
TAREHE 15 -09-2017
![]() |
WAZIRI MKUU WA UHISPANIA MARIANO RAJOY |
Waziri Mkuu
wa Uhispania, Mariano Rajoy leo anatarajiwa kwenda katika jimbo linalotaka
kujitenga la Catalonia, kutokana na hatua mpya ya viongozi wa kundi linalotaka
kujitenga kuanzisha kampeni yao kuhusu kura ya maoni ya uhuru.
Jana jioni,
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont akiwa mbele ya viongozi wengine wa kundi
linalotaka kujitenga, pamoja na umati wa wafuasi 8,000 waliokusanyika
Tarragona, alitangaza kuanza rasmi kwa kampeni hiyo ya kura ya maoni ambayo
imepigwa marufuku na serikali ya Uhispania.
Rajoy anatarajiwa kukutana na wanachama wa
chama chake cha kihafidhina cha Popular mjini Barcelona na hatarajiwi kuhutubia
umati wowote wa watu.
Hata hivyo zaidi ya asilimia 70 wamesema
wanataka kufanyika kwa kura hiyo ya maoni. Meya wa Barcelona, Ada Colau amesema
kura hiyo itaruhusiwa kufanyika bila kujali uamuzi wa serikali kuu mjini
Madrid.
WAZIRI MKUU WA UHISPANIA MARIANO RAJOY ANATARAJIA KWENDA KATIKA JIMBO LINALOTAKA KUJITENGA LA CATALONIA
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments