KIMBUNGA MARIA KIMESABABISHA VIFO VYA WATU 7 HUKO PUERTO RICO.
TAREHE 21-09-2017
![]() |
MADHARA YA KIMBUNGA MARIA |
Kimbunga Maria kimekata umeme katika
kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5 huku kikiwa tayari kimesababisha vifo vya watu
7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu.
Abner
Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura alisema kuwa hakuna mtu
anayetumia umeme aliye na huduma hiyo hadi sasa.
Kituo cha
vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hiyo.
Kimbunga Maria kwa sasa kinaondoka
nchini Puerto Rico na kumepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili.
Baada ya kimbunga Maria kuipiga
Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia manyumbani mwao kuanzia saa kumi na
mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi.
KIMBUNGA MARIA KIMESABABISHA VIFO VYA WATU 7 HUKO PUERTO RICO.
Reviewed by safina radio
on
September 21, 2017
Rating:

No comments