KIONGOZI WA MYANMAR AHUTUBIA TAIFA NA KUZUNGUMZIA GHASIA NCHINI HUMO.




TAREHE 19-09-2017

KIONGOZI  WA  MYANMAR AUNG  SAN  SUU  KYI

Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi amelihutubia taifa ambapo amezungumzia ghasia zinazoendelea nchini humo dhidi ya ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rhakine.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa ghasia hizo mwezi uliopita, Aung San Suu Kyi amesema serikali yake inalaani vikali ukiukwaji wa haki za binaadamu na unyanyasaji unaofanywa kinyume cha sheria.

 Amesema wako tayari kuanza mchakato wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi wowote ambao wanataka kurejea nchini humo baada ya kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.


Suu Kyi mwenye umri wa miaka 72, na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ameitoa hotuba hiyo baada ya mataifa yenye nguvu duniani kuionya Myanmar kwamba inaweza ikakabiliwa na hatua, iwapo haitachukua hatua za kukomesha ukandamizaji unaofanywa dhidi ya jamii ya watu wachache wa Rohingya katika jimbo la Rakhine.
KIONGOZI WA MYANMAR AHUTUBIA TAIFA NA KUZUNGUMZIA GHASIA NCHINI HUMO. KIONGOZI   WA   MYANMAR   AHUTUBIA  TAIFA   NA  KUZUNGUMZIA    GHASIA  NCHINI  HUMO. Reviewed by safina radio on September 19, 2017 Rating: 5

No comments