WATANZANIA WAMETAKIWA KUWA NA TABIA YA KUOMBEA FIKRA ZAO KWA LENGO LA KUKOMBOA MAJIRA NA NYAKATI.
TAREHE 15-09-2017
Watanzania
wametakiwa kuwa na tabia ya kuombea fikra zao ili kukomboa majira na nyakati
pamoja na vitu vilivyokufa kiroho na kimwili kwani watu wengi wamekuwa
wakijushughulisha na kazi bila kufikia mafanikio.
Aidha
katika mwendelezo wa maombi ya ili kukombolewa kifikra pamoja na majira na nyakati za mtu
zilizokufa,redio safina kesho katika ukumbi ulioko mbauda jijini Arusha
itajikita katika kufundisha watu jinsi ya kukomboa fikra zao katika ulimwengu wa roho ili kila mmoja ajue ni namna gani ataweza
kukomboa uhai wa vitu vilivyokufa kiroho.
Katika
kuyabainisha mambo yanayoweza kufa imebainika kuwa ni pamoja na elimu
biashara,kilimo na ufugaji,tumbo la uzazi, ndoa, huduma na miradi mingine
ambapo kesho maombi ya nguvu yatafanyika ili kuyavika uhai.
Sambamba
na maombezi kufanyika watu wote wanashauriwa kuja na vielelezo vya kazi zao
pamoja na chumvi ambapo vitu hivyo vitaombewa kwa kitendo cha imani cha
kuyavika uhai ili kila mmoja aweze kufikia mafanikio aliyojiwelea.
Hata
hivyo iwapo mtu atashindwa kukomboa fikra,majira na nyakati zake ni vigumu
kumtumikia Mungu wala kufanikiwa kwenye shughuli yoyote.
WATANZANIA WAMETAKIWA KUWA NA TABIA YA KUOMBEA FIKRA ZAO KWA LENGO LA KUKOMBOA MAJIRA NA NYAKATI.
Reviewed by safina radio
on
September 15, 2017
Rating:

No comments