MBUNGE WA CHAMA TAWALA CHA JUBILEE ATAKA JAJI MKUU NCHINI KENYA KUFUTWA KAZI
TAREHE 14-09-2017
![]() |
JAJI MKUU WA KENYA DAVID MARAGA |
Mbunge wa chama tawala cha Jubilee nchini
Kenya amewasilisha ombi la kutaka kufutwa kazi kwa jaji mkuu David Maraga.
Mbunge huyo wa Nyeri, Njiri Wambugu
amewasilisha ombi lake mbele ya tume ya huduma za majaji akidai kwamba jaji
Maraga alihusika katika kufanya makosa ya kutengua ushindi wa rais Uhuru
Kenyata.
Akihutubia vyombo vya habari, mbunge huyo
amedai kwamba Jaji huyo ''aliwashinikiza'' wenzake kubatilisha matokeo ya
uchaguzi wa rais Uhuu Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria mnamo
tarehe 1 Septemba mwaka huu mwaka huu.
Wambugu amefananisha ubatilishwaji wa
matokeo hayo ya urais na mapinduzi ya majaji na sasa anataka nia ya jaji Maraga
kuchunguzwa.
Wabunge wa chama cha Jubilee na rais Uhuru
Kenyatta wamekuwa wakiukosoa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo na
wameendelea na kuwataja majaji hao kuwa ''wakora''.
MBUNGE WA CHAMA TAWALA CHA JUBILEE ATAKA JAJI MKUU NCHINI KENYA KUFUTWA KAZI
Reviewed by safina radio
on
September 14, 2017
Rating:

No comments